IQNA

Hizbullah yalaani ugaidi Iraq na mauaji ya Waislamu Myanmar

14:13 - July 25, 2012
Habari ID: 2377229
Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon imelaani vikali hujuma za kigaidi hivi karibuni nchini Iraq ambapo watu zaidi ya mia moja waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa.
‘Sambamba na kulaani jinai hujuma hizi za kigaidi, Hizbullah ina matumaini kuwa uongozi wa Iraq utajitahidi kuimarisha umoja na mshikamano ili kukabiliana na itikadi ya kitakfiri ambayo inawafaidisha tu maadui ya Ummah wa Kiislamu,’ imesema taarifa ya Hizbullah.
Taarifa hiyo pia imewatuhumu vibaraka wa mashirika ya kijasusi ya kigeni kwa kuchochea machafuko Iraq .
Kundi la mtandao wa al-Qaeda, vibaraka wa chama cha Baath, makundi ya kukufurisha watu na vilevile vibaraka kutoka nje kama mashirika ya kijasusi ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Marekani ndiyo yaliyotajwa kuwa wahusika wakuu wa milipuko ya hivi karibuni mjini Baghdad.
Saudi Arabia ndio kinara wa nchi za Kiarabu ambazo zina uhusiano wa karibu na makundi amilifu ya kigaidi nchini Iraq.
Kuna ushahidi unaoonyesha kwamba, kuna mkono wa Saudi Arabia katika mashambulio mengi ya kigaidi ambayo yametokea nchini Iraq. Chuki ya Riyadh kwa serikali ya Baghdad na kutoridhishwa Saudia na muundo wa serikali ya Iraq zinatajwa kuwa sababu kuu za viongozi wa utawala wa Kifamilia wa Saudia za kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Aidha katika taarifa yake Hizbullah imelaani mauaji ya umati ya Waislamu wa Myanmar. Hizbullah imekosoa utawala wa Myanmar kwa kuwaua kinyama Waislamu wakiwemo watoto na wanawake na kuwatimua wengine wengi kutoka kwenye makazi yao.
1061478
captcha