IQNA

Tunisia yataka OIC ishughulikie Waislamu Myanmar

8:40 - July 29, 2012
Habari ID: 2379457
Serikali ya Tunisia imeitakaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuchukua hatua zenye maana kuhusu mauaji ya Waislamu nchini Myanmar.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Tunisia imesema OIC inapaswa kulaani vikali mauaji ya Waislamu huko Myanmar. Tunisia ni kati ya nchi ambazo zimeitisha kikao cha dharura cha OIC tarehe 15 Agosti mjini Jeddah kujadili kadhia ya Myanmar.
Katika wiki za hivi karibuni maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar. Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 katika nchi hiyo ya mashariki mwa Asia.
Nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu zinaendelea kunyamaza kimya licha ya jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar.
1064215
captcha