IQNA

Baniani asilimu katika kipindi cha televisheni Pakistan

8:33 - July 29, 2012
Habari ID: 2379461
Kijana wa Kibaniani amesilimu katika kipindi cha moja kwa moja cha televisheni nchini Pakistan.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyetambuliwa kwa jina la Sunil alikuwa miongoni mwa watu kadha ambao walisilimu tarehe 24 Julai katika kipindi hicho kilichokuwa kikirushwa hewani chini ya usimamizi wa Maulana Mufti Muhammad Akmal katika Kanali ya Televisheni ya Dijitali ya ARY.
Watu waliokuwa katika studio walimpongeza kijana huyo na kumpa mapendekezo kadhaa ya jina la Kiislamu na hatimaye iliafikiwa aitwe Mohammad Abdullah.
"Miaka miwili iliyopita, nilianza kufunga katika mwezi wa Ramadhani. Siko chini ya mashinikizo kuukubali Uislamu, nimeukubali Uislamu kwa khiari yangu," amesema kijana huyo.
Idadi ya Wahindu au Mabaniani Pakistan ni karibu asilimia 2.5 ya watu milioni 180 nchini humo.
1063787
captcha