Kwa mujibu wa tovuti ya CPI washiriki wa maandamano hayo ambayo yaliitishwa na Kamati ya Quds inayofungamana na Jumuiya ya Madaktari wa Kiarabu wametoa taarifa wakilaani vikali hatua ya utawala huo ya kutangaza kwamba leo utaingia katika msikiti huo muhimu na mtukufu kwa Waislamu.
Wamesema hatua yoyote ya utawala huo ya kutaka kuhujumu kibla hicho cha kwanza cha Waislamu itakabiliwa na radiamali kali ya Waislamu. Wameutahadharisha utawala huo usije ukadhani kwamba utafanya hujuma hiyo bila kupata jibu kali kutoka kwa wananchi wa Misri kwa sababu Misri ya leo ni tofauti kabisa na ile iliyokuwa ikitawaliwa na dikteta Hosni Mubarak aliyekuwa na urafiki mkubwa na utawala huo. 1064659