Kwa mujibu wa Fakhri Abu Diab, Jumapili iliyopita Jumuiya ya Misaada ya Silwan ilikuwa imeandaa futari ya umma katika hoteli ya Panorama eneo la Ras al Amud. Hata hivyo masaa mawili kabla ya kuanza futari hiyo, polisi ya Israel ilivamia eneo hilo na kusema kutokana na kuwa Jumuiya ya Silwan inapata msaada kutoka harakati za Kiislamu ikiwemo Hamas, hakuna ruhusa ya kuandaa futari.
Amesema mbali na kubatilishwa hafla hiyo ya kuwafuturisha wasiojiweza, polisi ya Israel pia iliwatia nguvuni viongozi wawili wa Jumuiya ya Silwan pamoja na mkurungezi wa Hoteli ya Panorama.
Utawala ghasibu wa Israel uliteka eneo la Quds Mashariki katika vita vya siku sita mwaka 1967. Utawala huo wa Kizayuni unadai kuwa Quds ndio mji wake mkuu.
Wapalestina wanaendeleza mapambano ya kuikomboa Quds na kusisitiza kuwa huo ndio mji mkuu wa dola huru la Palestina.
1065901