Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, chuo kimoja katika eneo la Mindanao mashariki mwa Ufilipino kimechukua uamuzi wa kibaguzi wa kuwazuia wanafunzi wa kike Waislamu kuvaa hijabu jambo ambalo ni ukiukwaji wa wazi wa haki za kuabudu.
Kufuatia uamuzi huo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Ufilipino Sheikh Ali Ayyub amesema jumuiya hiyo imeitaka shule hiyo kubatilisha uamuzi huo kwani unakiuka sheria za nchi na haki za binadamu.
Chuo cha Pilar mjini Mindanao kupitia mkuu wake Maria Nina Balbas kimesisitiza kuwa kitaendelea kutekeleza uamuzi wake huo wa kibaguzi. Chuo hicho kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki kimepuuza uamuzi wa baraza la mji wa kuruhusu hijabu katika shule zote.
Naye Rosemari Trajano Katibu Mkuu wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Ufilipino amekosoa vikali uamuzi huo na kusema haki ya kuabudu ni haki ya kimsingi ambayo haipaswi kukiukwa na chuo hicho cha Kikatoliki.
Ikumbukwe kuwa eneo la Mindanao ndio kitovu cha Uislamu nchini Ufilipino kwani Uislamu ulifika hapo karne ya 13 Miladia miaka 200 kabla ya Ukristo kufika nchini humo.
1068048