Rais Ahmadinejad aliyasema hayo Jumanne 31 Julai katika uzinduzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ya petroli cha Shahidi Tundguyan kusini mwa Tehran.
Akiendelea na hotuba yake Rais Ahmadinejad amesema kuwa hakuna nchi inayoweza kusimamisha harakati ya maendeleo ya taifa la Iran katika nyanja za sayansi na teknolojia. Ameongeza kuwa, taifa la Iran limeazimia kupiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.
Ahmadinejad ameendelea kusema kuwa mafuta ya petroli yamekuwa yakitumiwa na nchi kubwa duniani kama wenzo wa kisiasa wa wakoloni dhidi ya wazalishaji wa bidhaa biyo na kusema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafanya jitihada za kuhakikisha kwamba haiuzi tena nje mafuta ghafi.
Rais Ahmadinejad ameashiria siasa za nchi za kibeberu za kutaka kuhodhi teknolojia ya kutengeneza vipuri, kujenga viwanda vya kusafisha mafuta na kuwekeza katika sekta hiyo na akasema uzinduzi wa kiwanda cha Shahid Tundguyan cha kusafisha na kuboresha bidhaa ya mafuta ni sehemu ya jitihada za Iran za kuvunja siasa za Wamagharibi za kutaka kuhodhi teknolojia hiyo. Amesema kuwa umri wa fikra za kibeberu na kikoloni umefikia ukingoni na ameyausia mataifa ya kibeberu yabadilishe lugha yao wakati yanapotaka kuzungumza na taifa la Iran.
Amekanusha tena madai ya Magharibi kwamba Iran inataka kutengeneza silaha za mauaji ya umati na kusema taifa la Iran halina haja na silaha za aina hiyo na kwamba itaboresha uhusiano wake na nchi nyingine kwa kutumia mantiki, uadilifu, utamaduni, kupigania uhuru na ubinadamu.
1067244