Kwa mujibu wa gazeti la ad-Dastur linalochapishwa Jordan, iwapo jambo hilo litathibiti basi Wazayuni wataweza kuingia katika msikiti huo wakati wowote wautakao kwa kisingizio kwamba mabustani ni mali ya umma ambapo kila mtu anaweza kuingia humo kwa ajili ya kupumzika na kustarehe.
Akibainisha hatari ya hatua hiyo Kamal al-Khatib naibu mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Ardhi Zilizotekwa 1948, amesema kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel umeanza kutekeleza hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika mwezi huu wa Ramadhani na kwamba inatekelezwa kwa lengo la kufuta kabisa utambulisho wa Kipalestina katika mji mtakatifu wa Quds.
Wakati huohuo shakhsia wa kisiasa na kidini wa Palestina wamekuwa wakitoa ripoti zinazoonyesha kwamba utawala huo ghasibu umeongeza kasi ya kuharibu Msikiti wa al-Aqsa kwa kisingizio cha kulinda taasisi za Israel na kujenga eti hekalu la Nabii Suleiman (as). 1068057