Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa tangu mwaka 2000 White House na Tel Aviv zimekuwa zikifanya jitihada za kuipokonya silaha Hizbullah na kukomesha mapambano ya harakati hiyo dhidi ya Israel. Ameongeza kuwa lengo la wale wanaotaka Hizbullah iweke chini silaha zake ni kusimamisha mapambano ya harakati hiyo dhidi ya maghasibu wa Israel na kusema suala linaloilinda Lebanon kwa sasa ni mlingano wa nguvu baina ya Hizbullah na adui Mzayuni na kwamba Israel inaelewa kwamba endapo itaishambulia ardhi ya Lebanon kwa sasa italipa gharama kubwa. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza juu ya udharura wa kukombolewa ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu na Israel na ametoa wito wa kuwepo mazungumzo ya kitaifa kwa ajili ya kubuni stratijia ya kukomboa ardhi hizo.
1069136