IQNA

Mawakili Iran wataka Waislamu Myanmar wasaidiwe

17:08 - August 04, 2012
Habari ID: 2385242
Mawakili na wahadhiri wa taaluma ya sheria katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametoa taarifa wakitaka nchi zote za Kiislamu kuchukua hatua imara na za kivitendo kuhusu mauaji ya umati ya Waislamu wa kabila ya Rohingya nchini Myanmar.
Taarifa hayo imeukosoa vikali Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua kuhusu mauaji ya umati na ubakaji unaofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar.
Mawakili na wahadhiri wa taaluma ya sheria katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuwasilisha malalamiko makali ya Waislamu kuhusu jinai dhidi ya Waislamu Myanmar kwa jamii ya kimataifa.
Katika wiki za hivi karibuni maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar. Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 katika nchi hiyo ya mashariki mwa Asia.
Nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu zinaendelea kunyamaza kimya licha ya jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar.
1070520
captcha