Akibainisha mpango huo hapo jana Jumamosi mbele ya waandishi habari katika makao makuu ya muungano huo mjini Doha Qatar, Ali Muhyi Deen Qaradaghi, Katibu Mkuu wa muungano huo amesema kwamba mpango huo wa kuhubiri Uislamu barani Afrika tayari umeanza kutekelezwa. Amesema muungano huo wa wanazuoni wa Kiislamu unalipa suala la kuarifisha Uislamu barani Afrika umuhimu maalumu na kwamba una azma ya kuandaa kikao cha wanazuoni wa Kiislamu ili kupitisha stratijia ya utekelezaji wa mpango huo.
Amesema muungano huo utaainisha wahubiri wa kudumu 100 kwa lengo la kuhubiri Uislamu barani Afrika na kuwasihi watu wa bara hilo wajiepushe na vurugu na mivutano ya kimadhehebu. Amesema wahubiri hao wataanza shughuli yao hiyo muhimu barani Afrika katika hali ambayo wahubiri wa Kikristo wapatao laki saba tayari wanahubiri barani humo na kuwatwisha Waislamu itikadi zao potofu.
Mwishoni, Qaradaghi ameutaka umma wa Kiislamu zikiwemo serikali, kuwajali ndugu zao wa Kiislamu barani Afrika na kukidhi mahitaji yao. 1071285