Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema kuwa, kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) huko Makka hakitasaidia kutatua matatizo ya Syria kutokana na misimamo ya kiadui ya Saudi Arabia dhidi ya Damascus.
Alauddin Burujerdi amesema hayo leo na kusisitiza kuwa Jumuiya ya Nchi za Karabu (Arab League) na nchi kama vile Saudi Arabia zimekuwa na rekodi mbaya ya uadui dhidi ya Syria na kwamba kwa kuzingatia hilo haionekani kuwa kikao ha wakauu wa OIC huko Makka Saudi Arabia kitakuwa na natija ya kuridhisha ya kuutatua mgogoro wa Syria.
Burujerdi amesema Saudia imetoa pendekezo la kufanyika kikao cha jumuiya ya OIC huko Makka baada ya kufeli mpango wa kupunguza mivutano nchini Syria na kuongeza kuwa, Saudia imetumia uwezo wake wote kuvuruga amani na utulivu nchini Syria kwa kushirikiana na Arab League na baadhi ya pande za kieneo na madola ya kigeni kama vile Uingereza na Marekani.
1072564