IQNA

Mashindano ya Qur’ani Nigeria

18:00 - August 06, 2012
Habari ID: 2387031
Mashindano ya qiraa na hifdhi ya Qur’ani Tukufu yamefanyika katika Msikiti wa Ogunsanya mjini Lagos, Nigeria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yameandaliwa na Kundi la Nakomio kwa ushirikiano na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Nigeria pamoja na Taasisi ya Qur’ani ya Ahul Bayt AS.
Mashindano hayo yalianza kwa hotuba ya Sayyid Bagher Sayyid Javadi mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran.
Katika hotuba yake amezungumzia umuhimu wa kusoma na kuhifadhi Qura’ani Tukufu.
Naye Abdullah Anifuaz Mkuu wa Kituo cha Vijana wa Kiislamu Lagos amepongeza juhudi za Kituo cha Utamaduni cha Iran katika kuandaa program za Kiislamu na Qur’ani nchini Nigeria.
Washiriki 20 wanashiriki katika mashindano hayo ya Qur’ani. Pembizoni mwa mashindano hayo kulikuwa na maonyesho ya Qur’ani ambayo yaliwavutia watazamaji.
1071195
captcha