IQNA

Msafara wa misaada ya kibinadamu waelekea Gaza

17:19 - August 08, 2012
Habari ID: 2388711
Kundi moja la wanaharakati wa masuala ya kibinadamu kutoka Ulaya kaskazini (Scandinavia) limetuma meli ya misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa televisheni ya Press, wasimamizi wa msafara huo wanasema kwamba lengo lao ni kama la misafara iliyopita ambalo ni kuvunja mzingiro wa kinyama unaotekelezwa na uatawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Ukanda huo umekuwa chini ya mzingiro wa Wazayuni wa Israel tokea mwaka 2007, ambapo umeathiri pakubwa maisha ya wakazi wa eneo hilo kutokana na kiwango kikubwa cha umasikini na ukosefu wa ajira.
Pamoja na hayo, utawala wa Israel katika siku za hivi karibuni umepunguza mzingiro huo kwa kuruhusu baadhi ya bidhaa za dharura kama vile chakula na madawa kuingizwa katika ukanda huo. Hata hivyo bado mzingiro wa baharini dhidi ya ukanda huo unaendelea na kwa sasa hakuna bidhaa zinazoruhusiwa kusafirishwa nje ya ukanda huo. 1073945
captcha