IQNA

Amnesty International:

Kesi ya wapinzani Bahrain ni maskhara ya vyombo vya sheria

11:13 - August 13, 2012
Habari ID: 2391601
Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limetoa taarifa likikosoa hukumu zilizotolewa na mahakama za Bahrain dhidi ya wapinzani 13 wa serikali ya nchi na kuwataka maafisa wa nchi hiyo kukomesha maskhara ya vyombo vya sheria.
Kituo cha habari cha Lemonde kimeripoti kuwa Amnesty International imewataka viongozi wa serikali ya Bahrain kutayarisha mazingira ya kuachiwa huru wapinzani 13 wa serikali wanaotuhumiwa kwa kula njama dhidi ya serikali na kutoa hukumu ya kuachiwa huru.
Taarifa ya Amnesty International imesema kuwa, serikali ya Manama inapaswa kuhitimisha maskhara hayo ya vyombo vya sheria na mahakama za nchi hiyo na kufuta hukumu zilizotolewa dhidi ya wanamapambano 13 wanaopinga serikali bila ya masharti yoyote.
Mkurugenzi wa Amnesty Internationa kanda ya Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika Hassiba Hadj Sahraoui amesema kuwa watu hao 13 wamehukumiwa kifungo kwa sababu ya itikadi zao na walikamatwa kwa kosa la kutumia haki yao ya uhuru wa kusema na kupinga serikali.
Mahakama ya Bahrain inatazamiwa kutangaza hukumu dhidi ya kundi la wanaharakati wa haki za binadamu wa nchi hiyo Jumanne ya kesho. 1076554



captcha