IQNA

Viongozi wa dini za mbinguni walalamikia matamshi ya dharau ya mbunge wa Marekani

15:59 - August 13, 2012
Habari ID: 2392055
Matamshi ya dharau ya hivi karibuni ya Joe Walsh mbunge wa Congress ya Marekani dhidi ya Uislamu yameamsha hasira ya viongozi wa kidini nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya theonline, mbunge huyo wa Illinois wiki iliyopita aliwatuhumu Waislamu kuwa ndio waliohusika na tukio la Septemba 11 na matukio mengine kama hayo nchini humo na kuwataja kuwa tishio kubwa kwa usalama wa nchi hiyo.
Katika matamshi yake hayo ya kichochezi, Walsh alidai kwamba tishio la usalama la Waislamu kwa usalama wa Marekani ni kubwa zaidi sasa kuliko hata wakati wa Septemba 11 na kuwatuhumu kuwa wanafanya ugaidi kwa lengo la kuwaangamiza Wamarekani!
Kufuatia matamshi hayo yasiyo na msingi, viongozi wa Kikristo na Kiyahudi wameandaa mkutano wa waandishi habari katika ofisi za Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani mjini Chicago na kusema kuwa matamshi kama hayo ya dharau dhidi ya Uislamu ndiyo yanayoeneza fikra za chuki dhidi ya Uislamu katika jamii ya Marekani na kuhatarisha usalama wa misikiti ya Waislamu nchini humo.
Washiriki wa mkutano huo wa waandishi habari pia wamemtaka Walsh kufutilia mbali matamshi yake hayo na kuwaomba radhi rasmi Waislamu kutokana na matamshi hayo.
Akizungumza katika mkutano huo, Dhahir Sahlul, mkuu wa baraza lililotajwa, amesema kutuhumiwa Waislamu kuwa ni magaidi ni ishara ya wazi ya matamshi ya ubaguzi wa rangi ya Walsh. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, Waislamu wa Marekani wanapata watu milioni 7. 1076899
captcha