Muhammad Sabiih amesema kuwa kikao hicho kitatoa kipaumbele cha kwanza kwa suala la Quds tukufu na kwamba wakati umefika sasa kwa nchi zote za Kiislamu kufanya jitihada kubwa za kulinda Quds, matukufu ya Kiislamu ya Palestina na Msikiti wa al Aqsa mbele ya hujuma na siasa za Israel za kutaka kuliyahudisha eneo hilo.
Muhammad Sabiih amesema Israel inaendeleza siasa chafu za kuwalazimisha Wapalestina kukimbia makazi yao huko Quds na kujenga maabadi ya Kiyahudi katika eneo la Msikiti wa al Aqsa.
Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema Msikiti wa al Aqsa unakabiliwa na mzingiro mkali na hujuma za mara kwa mara za askari wa Israel na uchumbaji unaofanywa na utawala huo chini ya msikiti huo mtakatifu.
Kikao cha dharura cha viongozi wa nchi za Kiislamu kimenza leo mjini Makka ambako kinajadi masuala muhimu ya kieneo na jinsi ya kukabiliana nayo. 1078582