Ujumbe huo ambao umendikwa kwa lugha ya Kiingereza ni jibu kwa ukatili unaofanywa na Mabudha wa Myanmar katika jimbo la Arakan dhidi ya Waislamu na unasisitiza juu ya kusimamisha mauaji yanayofanwa dhidi ya wafuasi wa dini hiyo.
Ujumbe huo uliowekwa kwenye ukurasa wa mbele ya tovuti ya Wizara ya Habari ya Myamnar umesisitiza kuwa, Waislamu wanabeba ujumbe wa amani kwa ajili ya walimwengu lakini Mabudha wanawaua. Umetishia kuwa iwapo mauaji hayo yataendelea mabudha watalengwa kote duniani na nchi ya Myanmar itakuwa kama moto wa Jahannam.
Kandokando ya ujumbe huo kuna picha za maiti zilizochomwa katika eneo lisilojulikana.
Maelfu ya Waislamu wa Myanmar wameuawa na malaki ya wengine kufukuzwa katika makazi yao kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Mabudha wa nchi hiyo wakisaidiwa jeshi la serikali. 1077913