Nchi hizo ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Bahrain, Kuwait, Jordan, Palestina na Imarati zimetangaza kuwa leo Jumamosi ni siku ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa msingi huo Idul Fitr itasherehekewa hapo kesho Jumapili ambayo ni tarehe Mosi Shawwal.
Kwa kufungua kesho nchi hizo zitakuwa zimekamilisha siku 30 za funga kwa sababu zilianza kufunga siku ya Ijumaa tarehe 20 Julai kinyume na nchi nyingine za Kiislamu ambazo zilianza kufunga siku moja baadaye yaani siku ya Jumamosi. 1081310