Kwa mujibu wa tovuti ya Palestine Infor, washiriki wa maandamano hayo ambayo yaliandaliwa na wafuasi wa vyama vya kitaifa na Kiislamu walibeba mabango na bendera zilizokuwa na maandishi yanayounga mkono na kutetea matukufu ya Kiislamu na hasa Quds Tukufu.
Akizungumza katika maandamano hayo Rubah Mihna mmoja wa wanachama wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO amesema ni muhali ukombozi wa Palestina kupatikana kupitia mazungumzo yasiyokuwa na maana na Wazayuni pamoja na waungaji mkono wao wa Magharibi.
Amemtaka Mahmoud Abbas, kiongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina asimamishe mara moja ushirikiano wake wa kiusalama na utawala ghasibu wa Israel na kushirikiana na Wapalestina wengine katika kupambana na jinai za utawala huo dhidi ya taifa la Palestina. 1081276