Mawaziri na viongozi mbalimbali kutoka nchi 120 wanachama wa NAM na nchi 18 zisizo wanachama wa harakati hiyo pamoja na taasisi nyingine 10 za kimataifa wanakutana katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB.
Siku mbili zilizopita kulifanyika mkutano wa wataalamu wa kuandaa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje ambao utaandaa mazingira ya kufanyika mkutano wa wakuu wa harakati hiyo.
Mkutano wa viongozi hao unatarajiwa kufanyika alkhamisi na Ijumaa wiki hii hapa Tehran.
1086787