Kongamano la kimataifa la mazungumzo ya kisiasa na kidini limeanza leo katika mji wa Sarajevo huko Bosnia Herzegovina likisimamiwa na Jumuiya ya Sant' Edigio, Kanisa Katoliki la Sarajevo, Kanisa la Orthodox, Waserbia na jamii za Kiislamu na Kiyahudi za Bosnia.
Kongamano hilo muhimu linasisitiza juu utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini zote na ni la kwanza kufanyika katika eneo la Balkan kati ya viongozi wa kisiasa na kidini tangu baada ya vita vya eneo hilo katika muongo wa 1990.
Kongamano hilo la kimataifa la amani limefanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzingirwa mji wa Sarajevo na Waserbia miaka wa 20 iliyopita.
Kongamano hilo la siku mbili litakalokamilisha kazi zake kesho linahudhuriwa na viongozi wa dini mbalimbali na maafisa wa masuala ya utamaduni na ya kiraia kutoka nchi za eneo la Balkan na nchi nyingine duniani.
Kongamano hilo linatoa ujumbe kwamba mazungumzo kati ya dini na tamaduni tofauti ndiyo njia pekee ya kuwadhaminia wanadamu mustakbali bora. 1095714