IQNA

Sayyed Nasrullah asema Uislamu umewafelisha maadui

18:00 - September 17, 2012
Habari ID: 2413675
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah, ameutaka Umoja wa Mataifa upasishe azimio la kulinda matukufu ya dini za Mwenyezi Mungu.
Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo jana na kulaani njama za Marekani na utawala haramu wa Israel katika kutengeneza filamu chafu inayomdhalilisha Mtume Muhammad (saw). Amesema, katika hali kama hii nchi za Kiislamu zinatakiwa kufanya juhudi kubwa za kuulazimisha Umoja wa Mataifa upitishe azimio la kulinda matukufu ya dini za Mwenyezi Mungu. Akiashiria fatwa ya kihistoria iliyotolewa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomein dhidi ya murtadi Salman Rushdie, aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW mwandishi wa kitabu cha "Aya za Shetani" Sayyid Nasrullah amesema, hivi sasa vitendo vya kutusiwa matukufu ya Kiislamu vimeongezeka na kwamba, umma wa Kiislamu unayohistoria ya kulinda matukufu yake. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, kumtetea mtukufu Mtume Muhammad (saw) kuna maana ya kuyatetea matukufu yote, dini zote na Mitume wote wa Mwenyezi Mungu. Kwa upande mwingine Sayyid Hassan Nasrullah amesema, lengo la utengenezwaji wa filamu iliyomvunjia heshima mtukufu Mtume Muhammad (saw), ni kuzusha fitna kati ya Waislamu na wakristo na kwamba, njama hizo zimegonga mwamba na kufeli.
1100003
captcha