IQNA

Hujuma dhidi ya Uislamu inatishia amani ya kimataifa

23:59 - September 18, 2012
Habari ID: 2414735
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amesema kuwa vitendo viovu mithili ya filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) vinatishia amani na usalama wa kimataifa.
Ekmeleddin Ihsanoglu amesema kuwa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa OIC utakaofanyika wiki ijayo mjini New York utajadili suala hilo.
Ihsanoglu amewaambia waandishi habari mjini Jeddah kwamba OIC itatumia nguvu zake zote za kisiasa kukomesha vitendo hivyo viovu kwa sababu havijeruhi hisia za kidini za Waislamu pekee bali vinatishia usalama na amani ya dunia nzima.
Amesisitiza kwamba ghasia za sasa zimetokana na hisia zilizozushwa na filamu ambayo imewakosea heshima Waislamu kote duniani.
Katibu Mkuu wa OIC amesisitiza kuwa matukio yaliyojiri Benghazi, Khartoum, Cairo na kwengineko yamenesha matokeo ya kutumia vibaya uhuru wa kusema na kujieleza.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watakutana pambizoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 27 Septemba. 1101225
captcha