Akihutubia idadi kubwa ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Sidiqqi ameashiria vitendo vichafu vya kuvunjiwa heshima Mtume SAW katika nchi za Magharibi na kusema wanaotekeleza maovu hayo wana wasi wasi kuhusu hatua ya mataifa kuiga mfano wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuenea mwamko wa Kiislamu uliopelekea kutimuliwa madikteta vibaraka wa Magharibi katika nchi za Kiarabu. Amesema mwamko wa Kiislamu utadhoofisha madola hayo ya Magharibi.
Ayatullah Siddiqi ametoa wito kwa Waislamu na nchi za Kiislamu kudumisha umoja ili kukabiliana na wanaohujumu matukufu ya Kiislamu. Aidha amezitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua za pamoja ili kuishinikiza jamii ya kimataifa ikabiliane na wanaomvunjia heshima Mtume SAW.
Kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran, Ayatullah Siddiqi amesema hatua ya baadhi ya nchi kupinga mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani ni kisingizio tu cha kujaribu kuzuia ustawi wa Iran katika sayansi na teknolojia.
1103368