IQNA

Waziri wa kwanza Mwislamu ateuliwa Norway

5:05 - September 25, 2012
Habari ID: 2418911
Mwanamke Mwislamu ameteuliwa kuwa waziri wa utamaduni nchini Norway na hivyo kuwa Mwislamu wa kwanza kuteuliwa kuwa waziri katika nchi hiyo ya Skandinavia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waziri Mkuu wa Norway Jens Stoltenberg amesema: 'Tumefanya mabadiliko haya ili kutoa mwanya kwa thamani mpya, nguvu mpya na fikra mpya.'
Hadia Tajik , Mwislamu mwenye umri wa miaka 29 ameteuliwa kuwa Waziri katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanyika Septemba 22.
Tajik amechukua nafasi ya Anniken Huitfeldt ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Leba na Masuala ya Jamii.
Waziri wa Tajik ni Wapakistani nay eye ni mbunge wa Chama cha Leba.
Tajik ambaye ni waziri mwenye umri wa chini kabisa katika nchi hiyo ya Skandinavia amesema suala la kuleta maelewano baina ya tamaduni mbali mbali litapewa umuhimu katika wizara yake.
Kuna karibu Waislamu laki moja na nusu kati ya watu milioni moja na nusu Norway. Aghalabu ya Waislamu wa nchi hiyo ya Ulaya ni wa asili ya Pakistan, Somalia, Iraq na Morocco.
1105570
captcha