Ayatullah Emami Kashani sambamba na kulaani filamu hiyo, amesema mwamko wa Kiislamu unaoendelea kushuhudiwa kwa sasa hauwezi kuzimwa na yeyote.
Akizungumzia vitisho vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran, Ayatullah Kashani amesema taifa hili halitasita kuwapondaponda mazayuni iwapo watathubutu kuchukua hatua ya kipumbavu ya kuishambulia nchi hii.
Amesema kwa sasa Iran ya Kiislamu ipo katika jihadi ya kisiasa, kielimu na kiuchumi na wala haina muda wa kupoteza kupiga ngoma za vita usiku na mchana kama wanavyofanya Wazayuni. Hata hivyo ameonya kuwa shambulio lolote dhidi ya ardhi ya nchi hii litajibiwa kwa nguvu zote.
1108728