IQNA

Vikosi vya Saudia vyamuua shahidi mwandamanaji

15:10 - September 30, 2012
Habari ID: 2422429
Vikosi vya jeshi la utawala wa kifalme wa Saudi Arabia vimemuua shahidi kijana aliyekuwa na umri wa miaka 16 aliyekuwa akiandamana katika eneo la Awamiyya mashariki mwa nchi hiyo.
Kijana huyo alipigwa raisasi Jumatano iliyopita katika maandamano na kupoteza maisha yake Ijumaa ya wiki hii kutokana na majeraha aliyopata.
Siku ya Jumaosi ya jana pia vikosi vya jeshi la Saudia viliwafyatulia risasi waandamanaji katika mji wa Qatif ulio umbali wa kilomita 418 mashariki mwa mji mkuu, Riyadh. Waandamanaji walikuwa wanatoa nara dhidi ya serikali huku wakitaka utawala wa kifalme wa Aal Saud upinduliwe.
Tangu mwezi Februari mwaka jana wapinzani wa utawala wa Aal Saud wamekuwa wakifanya mudhahara na maandamano katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, wakitaka kufanyiwa marekebisho muundo wa utawala, kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa, usawa na mengineyo. Maandamano hayo sasa yamepanuka na kushuhudiwa katika miji mingine kadhaa ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Watawala vibaraka wa Saudi Arabia wanapata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa nchi za Magharibi hasa Marekani
1109529
captcha