Ekmeleddin Ihsanoglu amesema hayo katika radiamali yake dhidi ya filamu iliyotengenezwa na kusambazwa nchini Marekani inayomdhalilisha Mtume SAW.
Amesema Umoja wa Mataifa sambamba na kuheshimu matukufu ya dini na kuelewa masuala yanayopewa kipaumbele na ulimwengu wa Kiislamu, unapaswa kupasisha sheria zinazopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na kutangaza kwamba ni jinai kuuhujumu Uislamu.
Ihsanoglu amesisitiza kwamba, ubaguzi na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu vinatokana na uadui uliopo dhidi ya Uislamu na kwamba unakinzana na uhuru wa kusema ambao unadhaminiwa na sheria za kimataifa. 1109433