IQNA

Wamisri wajibu dharau ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu

15:48 - September 30, 2012
Habari ID: 2423063
Gazeti la al Watan linalochapishwa nchini Misri limejibu dharau na hujuma ya Wamagharibi dhidi ya Mtume wa Uislamu kwa kuchapisha katuni ya kuvutia inayokosoa mwenendo wa nchi za Magharibi kuhusu ulimwengu wa Kiislamu.
Baada ya kuchapishwa kibonzo hicho katika gazeti la al Watan, watumiaji wa mtandao wamekieneza kwa haraka na kwa wingi katika tovuti mbalimbali na kuwavutia watu wengi duniani.
Kibonzo hicho kina miwani ambayo vioo vyake viwili vinaonesha majengo mapacha ya Kituo cha Biashara ya Dunia cha New York yakiteketea kwa moto na chini yake kuna maandishi yanayosomeka: "Miwani ya Kimagharibi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu".
Al Watan limeandika kuwa limechapisha kibonzo hicho kujibu hatua ya jarida la Kifaransa lililochapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na kwamba kibonzo hicho hakikejeli au kumvunjia heshima mtu yeyote. Limeandika kuwa ujinga wa Wamagharibi wakati wanapozungumzia Uislamu unawavisha miwani inayowaonyesha tu tukio la Septemba 11, mwaka 2001. 1108764
captcha