IQNA

Mara hii Msyria wa Norway amvunjia heshima Mtume (saw)

19:39 - October 02, 2012
Habari ID: 2424698
Sara Azmeh Rasmussen, Msyria aliye na uraia wa Norway na ambaye ni mpinzani mkubwa wa mafundisho ya kidini na serikali ya Rais Bashar Asad wa Syria amesambaza katika weblogi yake picha chafu zinazomvunjia heshima moja kwa moja Mtume Mtukufu (saw).
Kwa mujibu wa tovuti ya challenge, mwandishi huyo ambaye pia ni msagaji amesema kuwa amesambaza picha hizo za vikatuni kwa ajili ya kuunga mkono hatua iliyochukuliwa hivi karibuni na jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha vikatuni vya kumdhalilisha Mtume Muhammad (saw).
Mwandihi huyo ambaye anadai kuwa ni Mwislamu amesema kwamba, haitoshi kutetea uhuru wa kwa maneno matupu bali yanapasa kuandamana na vitendo. Amesema bila aibu kwamba Waislamu wenyewe wanapasa kuchapisha na kusambaza duniani picha zaidi za Mtume (saw) ili eti kuimarisha uhuru wa kusema!
Mwandishi huyo wa weblogi ambaye katika maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani mwaka 2009 alichoma hadharani vazi lake la hijabu, ameazimia kujijengea nafasi miongoni mwa makundi yanayopiga vita Uislamu kwa kusambaza picha zinazomvunjia heshima Mtume (saw).
Kwa kuungwa mkono na baadhi ya watu wanaodai kuwa ni Waislamu, mwanamke huyo mwovu ameazimia kubainisha wazi zaidi nafasi yake ya kupinga mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu kwa kuchapisha na kusambaza picha zinazoyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 1111843
captcha