IQNA

Mahakama Kenya yapiga marufuku Hijabu, Waislamu kukata rufaa

22:17 - October 02, 2012
Habari ID: 2424757
Hivi karibuni mahakama moja nchini Kenya ilitoa uamuzi wa kushangaza pale ilipopiga marufuku uvaaji wa Hijabu shuleni na punde baada ya uamuzi huo Baraza Kuu la Waislamu Kenya SUPKEM limesema litakata rufaa katika mahakama huu nchini humo.
Kesi ilikuwa imewasilishwa mahakamani na wanafunzi Waislamu wa shule ya wasichana ya Kenya High ya mjini Nairobi ambao walikuwa wanalalamika kuwa uongozi wa shule uliwazuia kuvaa hijabu. Katika uamuzi wake , jaji aliyesikiliza kesi hiyo alidai uvaaji hijabu shuleni unakiuka katiba.
Viongozi wa Kiislamu kwa upande wao wanasema uamuzi huo wa mahakama unakiuka katiba pamoja na amri iliyokuwa imetolewa na Wizara ya Elimu Kenya iliyosema vazi la Hijabu linaruhusiwa katika shule zote nchini humo. Bw. Hassan Ole Naado Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya Supkem katika mahojiano na IQNA amesema watawasilisha kesi katika mahakama ya rufaa kufuatia uamuzi huo wa kupinga hijabu. Ameongeza kuwa jaji aliyetoa uamuzi huo alitaja mfano wa kupigwa marufuku hijabu Ufaransa jambo ambalo linaonyesha mahakama za Kenya zinaanza kutekeleza sera dhidi ya Uislamu za nchi za Ulaya. Hasan Ole Naado amesema Makanisa Kenya yanapanga njama ya kudhoofisha Uislamu na ameonya kuwa jambo hilo litasababisha matatizo makubwa nchini humo.
1111884
captcha