IQNA

Wazayuni wafunga tena Msikiti wa Nabii Ibrahim (as)

16:11 - October 03, 2012
Habari ID: 2425334
Kwa mara nyingine tena Wazayuni wa Israel wamechukua uamuzi wa kufunga Msikiti wa Nabii Ibrahim (as) katika mji wa al-Khalil kwa kisingizio cha kudhamini usalama wakati wa kufanyika sherehe za Mayahudi, na hivyo kuwazuia Waislamu kuswali katika mji huo.
Kwa mujibu wa Zaid al-Ju'bari, mkuu wa ofisi ya wakfu ya Palestina, watawala wa Kizayuni waliwaandikia barua siku ya Jumatatu wakiwafahamisha kwamba msikiti huo utafungwa siku za Jumanne na Jumatano za wiki hii kwa sababu za kiusalama.
AL-Ju'bari amelaani vikali hatua hiyo ya Wazayuni na kusema kuwa huo ni uchokozi wa wazi dhidi ya matukufu ya dini za mbinguni. Ameongeza kuwa Wazayuni pia wamezuia kutolewa adhana katika msikiti huo wakidai kuwa sauti ya adhana inawakera maghasibu wa Kizayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina katika eneo la msikiti huo.
Al-Ju'bari ameongeza kuwa kwa kuweka vizuizi vya upekuzi na ukaguzi pamoja na kuwatoza ada Waislamu wanaotaka kuswali katika msikiti huo, Wazayuni wana lengo la kubana na kuwazuia Waislamu wasiingie kabisa katika msikiti huo.
Wazayuni huufunga msikiti huo mara kwa mara katika sherehe tofauti za walowezi wa Kiyahudi kwa kisingizio cha kulinda usalama wao wakati wa kufanyika sherehe hizo. 1112606
captcha