Jaji mmoja wa mahakama ya serikali kuu ya Marekani mjini Washington DC jana Ijumaa alikiruhusu kikundi kimoja cha Wazayuni kilicho na misimamo ya kupindukia mipaka kuweka mabango yaliyo na matangazo ya chuki dhidi ya Uislamu katika vituo vya treni ya chini kwa chini mjini humo.