IQNA

Maandamano dhidi ya serikali Saudi Arabia

6:58 - October 09, 2012
Habari ID: 2428183
Makumi ya maelfu ya wananchi wameandamana Jumapili usiku katika mji weenye utajiri wa mafuta mashariki mwa Saudi Arabia.
Huku wakitoa nara dhidi ya ukoo wa Aal Saud unaotawla nchini humo, waandamanaji hao wamelaani ukandamizwaji unaotekelezwa na vikosi vya usalama nchini humo.
Tokea Februari mwaka 2011 Saudi Arabia imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika historia ya utawala wa Aali Saud. Utawala wa Saudia umekuwa ukihaha na kutumia kila mbinu zikiwemo za ukandamizaji na mkono wa chuma ili kufanya hali ya mambo nchini humo kuwa kama unavyotaka.
Lakini hivi sasa hali inayonyesha kwamba, ni kinyume kabisa na matakwa ya viongozi na wana wa ufalme wa nchi hiyo. Sasa nchi hiyo sio kisiwa cha amani tena kwa watawala wa nchi hiyo. Vurugu na mapigano ya hivi karibuni baina ya vikosi vya usalama na waandamanaji katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ni jambo linaloonyesha dhahir shahir kwamba, ndoto za wana wa ufalme wa nchi hiyo zimo katika hali ya kugeuka na kuwa jinamizi la kuogofya. Mji wa Madina, Qatif, Awamiyah na As-saf'wah hivi karibuni imegeuka na kuwa uwanja wa mudhahara na maandamano dhidi ya serikali. Maandamano hayo, yamekabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
1115607
captcha