IQNA

Imam Khamenei: Iran imeimarika chini ya vikwazo

20:14 - October 12, 2012
Habari ID: 2429997
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maendeleo yote yaliyofikiwa nchini Iran yamepatikana wakati taifa hili likiwa chini ya vikwazo.
Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo leo alipokutana na maelfu ya maulamaa, walimu na wajumbe wa bodi ya wahadhiri wa vyuo vikuu vya mkoa wa Khorasan Kaskazini huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Akiashiria ongezeko la kiwango cha uzalishaji wa elimu nchini Iran uliofikia kiwango cha asilimia mbili duniani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maendeleo yote haya yamepatikana katika vipindi vigumu vya vikwazo na kwamba, maendeleo hayo yamepatikana kwa juhudi zisizo na kifani za vijana wenye vipawa wa taifa hili. Aidha Ayatullah Ali Khamenei amesema, vituo vya takwimu vyenye itibari duniani vimeiweka Jamhuri ya Kiislamu katika nafasi ya 16 kielimu na kwamba vituo hivyo vimetabiri kuwa katika miaka sita ijayo, nafasi hiyo itapanda na kufikia ya nne. Akisisitiza juu ya ulazima wa kulipa umuhimu suala la kuwaandaa kimalezi watoto ili wawe na utambulisho wa kiutu wenye hulka na silka njema kuanzia kwenye kipindi cha utotoni, Kiongozi Muadhamu amesema, hitajio la msingi la Iran ni kujenga moyo wa matumaini juu ya mustakbali na kukifanya kizazi cha vijana kiwe na moyo wa kujiamini.
1117748
captcha