IQNA

Waislamu Uganda, DRC marufuku kuhiji mwaka huu

19:55 - October 20, 2012
Habari ID: 2434778
Serikali ya Saudi Arabia imesema Waislamu wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu kutokana na kuibuka ugonjwa wa Ebola katika nchi hizo mbili za Afrika.
Kiongozi wa Jamii ya Waislamu Congo Sheikh Abdallah Mangala ameelezea masikitiko yake kuwa Waislamu wa nchi hizo hawataweza kushiriki katika ibada ya Hija.
Tokea mwezi Agosti mwaka huu watu 74 wamepatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Congo ambapo nusu yao wameaga dunia. Nchini Uganda watu 17 wamepoteza maisha tokea mwezi Julai baada ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Wakati huo huo duru kutoka Saudi Arabia zinasema zaidi ya mahujaji milioni moja tayari wameshawasili nchini humo.
Wakati huo huo serikali ya Uganda imetangaza kuwa Ijumaa ijayo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa kwa ajili ya Sikukuu ya Idul Adh'ha itakayoadhimishwa kote duniani.
Msemaji wa Wizara ya Huduma za Umma Jonas Tumwine amesema serikali ya Uganda imeitangaza siku ya Idul Adh'ha kuwa siku ya mapumziko baada ya kushauriana na viongozi wa Kiislamu.
1122860
captcha