Waislamu wasiopungua 11 wa kabila la Rohingya wameuawa nchini humo baada ya mabudha wenye misimamo mikali kuchoma moto nyumba zao katika vijiji vya Waislamu mjini Sittwe, katika mkoa wa Rakhine wa magharibi mwa Myanmar.
Ukatili na mauaji hayo dhidi ya Waislamu yametokea baada ya kundi la mabudha likisaidiwa na jeshi la Myanmar pamoja na vikosi vya mpakani kuchoma moto nyumba za Waislamu katika vijiji vya Mamra na Mraut.
Jeshi la Myanmar limeripotiwa kuwapa mitungi ya petroli mabudha hao wenye misimamo mikali ili wakachome moto nyumba za Waislamu hao kwa lengo la kuwalazimisha kuhama kwenye vijiji vyao.
Ukatili huo mkubwa dhidi ya Waislamu unafanyika huku mashirika yanayodai kutetea haki za binaadamu duniani yakiendelea kunyamazia kimya ukatili huo.
1124664