IQNA

Mahujaji wa Nyumba ya Allah waelekea Mina

21:42 - October 23, 2012
Habari ID: 2436890
Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, al Kaaba leo wameelekea Mina kwa ajili ya kutekeleza marasimu na ibada ya siku ya Tarwiya hiyo kesho tarehe 8 Dhilhaji katika eneo hilo tukufu.
Ripoti zinasema kuwa mahujaji kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuelekea Mina jioni ya leo wakiwa katika makundi makundi chini ya ulinzi wa vyombo vya usalama vya Saudi Arabia. Mahujaji watakesha katika uwanja wa Mina na jioni ya tarehe 8 watafunga safari kuelekea Arafa kwa ajili ya kutekeleza nguzo kuu ya hija tangu alfajiriya siku ya tarehe 9 Dhilhaji.
Mina ni ardhi kubwa iliyoko baina ya silsila ya milima miwili karibu na Mash’arul Haram na mji wa Makka.
Mamilioni ya mahujaji kutoka nchi mbalimbali tayari wamewasili Makka na hadi sasa inaripotiwa kuwa ibada ya hija mwaka huu inaendelea vyema na hakujatokea jambo lolote la kutia wasiwasi.
Saudi Arabia imewapiga marufuku mahujaji kutoka nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutekeleza ibada ya hija mwaka huu kutokana na hofu na ugonjwa wa Ebola uliotokea katika nchi hizo mapema mwaka huu. 1124668
captcha