IQNA

Maelfu ya mahujaji wajibari na washirikina

23:44 - October 26, 2012
Habari ID: 2437959
Maelfu ya wahujaji wa Kiirani na wasio Wairani wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu jana tarehe 9 Dhilhaji walishiriki katika amali ya kujitenga na kujiweka mbali na washishirikina iliyofanyika katika uwanja wa Arafa.
Amali hiyo ya kujitenga na washirikina ambayo ilifanyika kwa kaulimbiu ya "Labbaik ya Muhammad", iliambatana na nara za Mauti kwa Marekani na Mauti kwa Israel zilizokuwa zikitolewa na mahujaji kutoka nchi mbalimbali duniani.
Taarifa iliyotolewa na mahujaji hao imesisitiza juu ya kuimarishwa umoja na mshikamano kati ya Waislamu na kulaani vikali hujuma inayofanywa na nchi za Magharibi dhidi ya matukufu ya Uislamu hususan Mtume Muhammad (saw). Mahujaji hao pia wamesisitiza kwamba Palestina ndio suala kuu la ulimwengu wa Kiislamu na kutilia mkazo udharura wa kukombolewa kikamilifu ardhi inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni ya Palestina.
Vilevile wamelaani himaya na uungaji mkono wa pande zote wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel na kutoa wito wa kuhukumiwa watenda jinai wa Israel katika mahakama za kimataifa.
Mapema leo karibu mahujaji milioni nne wanaelekea Mina katika siku ya kwanza ya Idil Haji na kufanya amali ya kumpiga mawe shetani, kuchinja wanyama, kisha kunyoa nywele zao na kadhalika. 1126143
captcha