Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina amesema kuwa utawala wa Israel unazidi kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina na ameitaka jamii ya kimataifa isusie na kuyawekea vikwazo makampuni yanayojishughulisha na ujenzi katika maeneo hayo.