IQNA

Iran yataka Myanmar iheshimu haki za Waislamu

11:58 - October 28, 2012
Habari ID: 2438982
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka serikali ya Myanmar kulinda haki za kimsingi za Waislamu nchini humo.
Katika taarifa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast ameelezea wasi wasi wa Tehran kuhusu hujuma za Mabuddha wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.

Mehmanparast amesema Iran iko tayari kutoa msaada kwa serikali ya Myanmar kwa lengo la kumaliza machafuko ya kikabila na kidini nchini humo. Ameelezea matumaini yake kuwa Myanmar itachukua hatua za kuhakikisha Waislamu na Mabuddha wanaishi kwa amani nchini humo.

Katika siku za hivi karibuni makumi ya Waislamu wa Myanmar wameuawa katika hujuma zinazotekelezwa na Mabuddha wakisaidiwa na vikosi vya serikali. Tokea mwezi Juni mwaka huu, maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na Mabudha huku makumi ya maelfu ya wengine wakiachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka katika jimbo la Rakhine mashariki mwa Myanmar.
1127235
captcha