Kiongozi Muadhamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo Jumatano hii mjini Tehran alipokutana na maelfu ya wanachuo na wanafunzi tofauti katika kukaribia kwa tarehe 13 Aban sawa na tarehe 4 Novemba, ambayo hapa nchini Iran inahesabiwa kuwa ni siku ya taifa ya wanafunzi na kupambana na ubeberu wa kimataifa. Kiongozi Muadhamu amewataka viongozi na wakuu wa mihimili mitatu ya dola yaani serikali, bunge na mahakama nchini Iran, kufanya kazi kwa bidii na kwamba katika kipindi hiki wanatakiwa kuwa makini katika utendaji wa kazi zao na wajiepushe na masuala madogomadogo yanayoenezwa na makelele ya vyombo vya habari vya Wamagharibi.
1129888