Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema kuwa, katika kipindi cha miaka 33 iliyopita, taifa la Iran limeweza kushinda njama zote za Wamagharibi za kuizuia Jamhuri ya Kiislamu isifikie hatua ya kujitosheleza katika nyanja mbalimbali.
Sayyid Muhammad Husseini amesema hayo akizungumza kwa mnasaba wa Sikukuu ya Ghadir iliyoadhimishwa kote duniani leo na kusisitiza kwamba, licha ya kuwa maadui wamefanya njama nyingi ili kuizuia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isifikie hatua ya kujitosheleza, lakini taifa hili kwa kudumisha umoja na kufuata Wilaya na uongozi limezishinda njama zote za maadui. Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema Wamagharibi wana woga na wahaka mkubwa wa maendeleo ya nchi nyingine na ndio maana wamekuwa wakifanya njama za kuusambaratisha mfumo wa Kiislamu hapa nchini; lakini inaonekana juhudi zao hizo ni sawa na za mfa maji ambaye haachi kutapatapa.
1130539