Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran, Hujjatul-Islam Kadhim Siddiqi amesema kuwa wananchi wa Syria wanakabiliwa na mashinikizo kutokana na harakati zao za muda mrefu za kupambana na utawala ghasibu wa Israel.
Hata hivyo amesisitiza kuwa haki itadhihirika nchini Syria na upande unaopigania haki utashinda. Hujjatul-Islam Siddiqi amesema inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wa eneo la Mashariki ya Kati wakiongoza kampeni za kuwapiganisha wananchi wa Syria na kuonya kwamba moto waliouwasha utasambaa na kuchoma nyumba zao pia.
Sheikh Siddiqi amesema nchi zinazounga mkono machafuko nchini Syria, zinafuata kibubusa malengo haramu ya Marekani.
Huku hayo yakijiri, makumi ya watu wamejeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia amewapongeza Waislamu kote duniani kwa kuwadia siku ya tarehe 18 Dhilhaji inayokumbusha tukio la kutangazwa rasmi Imam Ali bin Abi Twalib kuwa kiongozi wa umma wa Kiislamu baada ya Mtume Muhammad (saw). Amelitaja hatua ya Mtume (saw) ya kumtangaza Imam Ali (as) kuwa khalifa baada yake kuwa itabakia milele katika historia ya mwanadamu.
1130042