IQNA

Majalisi za Muharram zaanza Mombasa, Kenya

16:58 - November 17, 2012
Habari ID: 2449851
Jumuiya ya Tabligh ya Bilal Muslim Mission Kenya imetangaza kufanyika Majalisi katika siku 10 za mwezi wa Muharram katika mji wenye Waislamu wengi wa Mombasa nchini Kenya.
Katika taarifa, Bilal Muslim Mission imesema majalisi hizo zitafanyika katika Ukumbi wa Bilal mjini Mombasa.
Aidha majalisi zingine zitafanyika katika vijiji vilivyo karibu na mji wa Mombasa ambazo zitafanyia baada ya sala za Magharibi na Ishaa kwa ajili ya wanaume. Majalisi maalumu kwa ajili ya wanawake zitafanyika baada ya sala za Dhuhr na Asr. Aidha Jumuiya ya Tabligh ya Bilal Kenya imepanga maandamano katika Siku ya Ashura na vilevile kutakuwa na hotuba maalumu kabla ya sala ya Adhuhuri.
Jumuiya ya Tabligh ya Bilal Muslim Mission Kenya pia imesema imeandaa vipindi maalumu vya radio kuhusu Hamasa ya Karbala ambavyo vitarushwa hewani katika radio ya Pwani FM ye eneo la pwani ya Kenya katika miezi ya Muharram na Safar. Vilevile katika siku ya Ashura, kipindi maalumu cha radio kitarushwa hewani kote Kenya kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Kenya KBC.
1138939
captcha