Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza imeshapindukia mia moja wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.
Duru za hospitali za Palestina zimesema kuwa, Wapalestina 110 washauawa shahidi na zaidi ya elfu moja kujeruhiwa katika mashambulizi ya mfululizo ya utawala wa Kizayuni yanayoendelea kwa wiki nzima sasa huko Ghaza.
Mtoto wa miaka minne na ndugu yake wa miezi 18 pamoja na wazee wao ni miongoni mwa wananchi waliouawa shahidi jana kwenye mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza.
Katika upande mwingine, Marekani imesema kuwa itatumia kura ya veto dhidi ya muswada wowote utakaotumwa Umoja wa Mataifa kulalamikia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Kwa upande wao wanapambano wa Palestina jana walianza kutumia aina mpya ya makombora yanayofika maeneo ya mbali zaidi na kuwafanya maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wachanganyikiwe.
Redio ya utawala wa Kizayuni imesema kuwa, Israel imeomba kusimamishwe vita kwa muda wa masaa 24 hadi 48 ili ipatikane njia ya kuzungumzia suala la kusimamisha vita.
1140922