IQNA

Wazayuni wazidisha mashambulizi dhidi ya watu wa Gaza

22:18 - November 21, 2012
Habari ID: 2452826
Wapalestina wasiopungua 151 wameuawa shahidi na wengine 1,200 kujeruhiwa katika kipindi cha wiki moja ya hujuma ya utawala wa haramu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
Duru za habari Palestina zinasema idadi kubwa ya waliouawa na kujeruhiwa ni wanawake na watoto.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada Kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA limeashiria hali mbaya katika Ukanda wa Ghaza na kusema nusu ya wakazi milioni moja nukta saba wa eneo hilo ni watoto wadogo.
Israel imepata kiburi cha kuendeleza jinai zake baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kusema Washington inaunga mkono hujuma ya Tel Aviv dhidi ya watu wa Ghaza. Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ana azma ya kutumia udiplomasia kusimamisha mapigano yaliyoanzishwa na Israel katika Ukanda wa Ghaza. Ameyasema hayo mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan leo Jumatano wakati alipokutana na kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas. Kwingineko, maandamano yanaendelea katika maeneo mbalimbali duniani kulaani mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel huko Ghaza. 1141941
captcha