Akielezea ushindi wa wanamapambano wa Kipalestina mbele ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku nane huko Gaza, Hujjatulislam Kadhim Siddiqi ameongeza kuwa, ushindi wa wananchi wa Palestina umethibitisha kwamba, utawala wa Israel pamoja na kujigamba kwamba una nguvu za kijeshi, umeanza kudhoofika na hatimaye utatokomea kabisa. Akielezea kushindwa mfumo wa kujihami na makombora wa Israel kuzuia makombora ya Wapalestina, Hujjatulislam Siddiqi amesisitiza kuwa, uwezo wa makombora ya Wapalestina umeonyesha kuwa, mfumo huo wa wa Israel, hauna uwezo wa kuwalinda Wazayuni maghasibu. Sheikh Siddiqi amebainisha pia mauaji ya halaiki yaliyofanywa na majeshi ya Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza katika vita vya siku nane na kuongeza kuwa, mauaji hayo ya halaiki, yameonyesha wazi uwongo wa taasisi za kimataifa wa kudai eti zinatetea haki za binadamu. Katika sehemu nyingine, Siddiqi amezungumzia njama za maadui zinazofanywa dhidi ya wananchi na serikali ya Syria na kuongeza kuwa, baadhi ya nchi za Magharibi na hasa Marekani na zile za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na hata Uturuki zinatuma silaha kwa magaidi wa Syria kwa shabaha ya kutekeleza malengo haramu ya Israel na kutoa pigo kwa muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati, na kwamba bila shaka njama hizo zimegonga ukuta.
1145466