Ayatullah Muhammad Ali Mowahidi Kermani ameongeza kuwa, mgogoro wa hivi sasa wa Syria unatokana na uingiliaji wa baadhi ya madola ya kieneo na ya nje ya eneo hili katika masuala ya ndani ya nchi hiyo. Amesema madola hayo ya kigeni yanalenga kuiangusha serikali ya kisheria ya Rais Bashar Al Assad.
Ayatullah Kermani ambaye alikuwa akihutubia maelfu ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, amesisitiza kuwa watu wa Syria ndio wanaopaswa kuamua kuhusu hatima ya nchi yao. Amesema kuwatumia silaha na kuwaunga mkono waasi na makundi ya kigaidi nchini Syria ni jambo ambalo litazidi kurefusha mgogoro wa nchi hiyo.
Kuhusu hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kukamata ndege ya kijasusi ya Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Ayatullah Kermani amesema hiyo ni ishara ya uwezo mkubwa wa kiimani na kiteknolojia nchini Iran. Ameongeza kuwa kukamatwa ndege hiyo isiyo na rubani ni ishara ya kuwa Iran ina uwezo mkubwa zaidi ya Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, George Little amekiri kuwa ndege hiyo ya kijasusi aina ya ScanEagle imetengenezwa Marekani.
1149190